Sunday 24 April 2016

YOUTUBE YA BURE KUNUFAISHA WENGI


WATUMIAJI wa simu za mkononi wa kampuni ya Tigo Tanzania watanufaika na huduma ya bure ya mtandao wa YouTube ambapo wanaweza kutazama na kupakua video kutoka katika mtandao huo nyakati za usiku.
Mkuu wa Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano wa Tigo, David Zacharia alisema huduma hiyo itaanzia 6.00 usiku hadi saa 12.00 alfajiri.
Alisema,wateja wa Tigo pia wamepewa fursa ya kuweka video kwenye simu zao ambayo ni programu inayojulikana kama YouTube Offline inayomwezesha mtumiaji kuongeza video kwenye simu yake, ili aweze kuiangalia baadaye wakati ambapo muunganisho wa intaneti unakosekana au kuwa chini.
Ikiwa imeshachukuliwa kwa njia hiyo video inaweza kuchezeshwa bila kuunganishwa na intaneti kwa muda wa hadi saa 48, hivyo mtumiaji anaweza kuzifurahia video zake za YouTube bila hofu ya maunganisho na intaneti kuwa chini.
“Mteja anatakiwa kuwa na simu itakayomwezesha kuwa na data hizo za Offline kwa hiyo ni vema wakanunua simu yenye uwezo mkubwa wa intaneti,” alisema Zacharia.

Chanzo : Gazeti la Habari Leo.

No comments:

Post a Comment