Vijana wengi wamekuwa na Hamu ya kutaka kujiajiri ili waweze kujiingizia kipato kitakachoweza kuwasaidia kujikimu katika maisha yao. Ila ukosefu wa Mitaji umeonekana ni kikwako kikubwa sana katika harakati hizo za kujiajiri.
Vifuatavyo ni vitu ambavyo mtu ambaye hana mtaji anaweza akafanya na
akawa amejiari na kuweza pia kujipatia kipato Insha Allah.
1. Ufundi Stadi
Ufundi stadi ni ufundi ambao mtu anaweza kutengeneza kitu chenye kuvutia
na akauza kwa watu wengine watakaokipenda kitu hicho. Vipo vitu vingi ambayo
mtu anaweza kutengeneza kwa mikono yake na akapata kipato kidogo kinachoweza
kumfanya ajikimu na kikingine kuweka kama mtaji wa kukuzia bishara yake (Think Big).
Mtu
anaweza kutengeneza Fagio za Chelewa na kuuza mtaani. Pia vitu kama Makochi
(Sofa Ste), Mazulia ya kufutia Miguu, Dawa za Asili ni vitu ambavyo mtu anaweza
kujifnza kutengeneza na akaanza kuuza na kujipatia kipato cha kujikimu jata
kama hana mtaji.
2. Uza Vitu (au Huduma) kutoka kwa mtu Mwingine.
Hii ni njia nyingine ambayo mtu anaweza kujiajiri bila hata ya kuwa na
mtaji. Wapo watu (au wafanyabiashara) ambao wanatafuta watu wa kuwauzia bidhaa
zao kwa makubaliano ya kulipwa asilimia ya mapato (Commission) au hata kwa
kumuacha mtu auze bidhaa kwa bei anayotaka na kurudisha kiasi atakachoambiwa arudishe kwa
mwenye bidhaa.
Hapa mtu ahitaji mtaji wa aina yoyote zaidi ya nguvu zake na
muda wake wa kuuza bidhaa 9au huduma) husika.
3. Uza Maarifa.
Hakuna mwanadamu ambaye hana maarifa (isipokuwa wale wenye matatizo ya
akili). Mtu anaweza kuangalia maarifa aliyonayo kisha akayafanya kama mtaji na
kuwauzia wengine. Mtu anaweza kuanzisha mafunzo ya masomo ya ziada kwa
wanafunzi wa shule za msingi au sekondari na akaweka gharama ndogo za masomo hayo
na akapata kipato.
4. Badilishana na mtu kile ulichonacho.
Wengi wetu tunamiliki vitu kadhaa ambavyo vinathamani ambapo
vikibadilishwa na vitu vingine vinaweza kutupatia kiasi kidogo cha pesa
kinachoweza kutumika kama mtaji. Mfano wa vitu hivyo ni kama vile Simu za
Mkononi, Laptops, n.k. Mtu anaweza kubadilishana vitu hivi na Pesa (aidha kwa
kuuza au kuviweka Dhamana kwa muda) na akapata mtaji wa kuanzisha ajira yake
binafsi.
Hizo ni baadhi tu ya njia zinazoweza kutumika kama ajira binafsi na
kuweza kujiingizia kipato Insha Allah. Anza kuzitumia leo huku ukimuomba
Mwenyezi Mungu akuongoze na kukusimamia uzuri katika kuzitumia njia hizo.
Maassalaam
No comments:
Post a Comment